MKATE WA SINIA/ MKATE WA MCHELE/ MKATE WA KUMIMINA.
MAHITAJI
Mchele vikombe 2
Sukari kikombe kasoro robo 3/4
Hiliki 1 tsp
Hamira 2-3 tsp
Mafuta ya kupikia 2 tblsp
Tui la nazi vikombe 2 (kikombe utakachopimia mchele ndio upimie tui ) kila likiwa zito na mkate unakuwa laini zaidi.
MATAYARISHO
roweka mchele usiku mzima au angalau masaa 5.
Ukisha kurowana uchuje maji yote utie kwenye blender pamoja na hiliki na hamira usiweke sukari.
Tia na tui kikombe kimoja na nusu bakisha nusu. Halafu saga kwa dakika mbili.
Pumzisha mashine. Halafu saga tena. Saga mpaka uwe mzito. Lakini ubakie na chenga chenga kidogo.
Umimine kwenye bakuli la plastic. Chukuwa lile tui nusu lilobakia lichanganye na sukari halafu tia kwenye ule mchanganyiko wa mchele.
Mix kwa kutumia mwiko wa mbao au plastic, onja sukari kama iko sawa wacha uumuke.
Ukisha kuumuka. Weka frying pan juu ya jiko tia mafuta yakisha kupata moto. Ukoroge ule unga vizuri halafu umimine kwenye frying pan ufunike.
Watu wengine wanauwacha hapo juu ya jiko na moto mdogo mdogo mpaka uive. Halafu wanautia kwenye grill ufanye rangi juu.
Mie nauwacha hapa kwenye jiko kwa dakika mbili halafu nautia kwenye oven kwa moto mdogo mdogo. Mpaka uive uwe mkavu hautikisiki tena. Halafu nauweka kwenye grill upige rangi juu (hii njia ninofanya mie unakuwa hakuna chansi ya mkate wako kuunguwa chini) lakini fanya utakayoona rahisi kwako.
Ukiiva ENJOY.😃
Usisahau ku like na ku comment darling. Maoni yako ni muhimu kwetu.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni